Tanzania imelalamikia kitendo cha Kenya kupiga marufuku uuzwaji wa gesi nchini humo kutoka nchini Tanzania na kusambazwa kwa watumiaji wa Kenya.
Aidha, katika taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Prof. Adolf Mkenda imesema kuwa Serikali imeligundua suala hilo kupitia vyombo vya habari nchini humo.
Prof. Mkenda amesema kuwa kitendo cha Kenya kupiga marufuku uuzwaji wa gesi hiyo ni kwenda kinyume na mkubaliano ya umoja wa Afrika Mashariki wa kibiashara.
Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Kenya,aliliandikia barua Shirika la viwango nchini Kenya KBS kuwa hakuna gesi yeyote kutoka Tanzania itakayoingizwa kwaajili ya kuuzwa nchini humo.