TANZANIA imekwea kwa nafasi tatu kutoka nafasi ya 135 mpaka nafasi ya 132 katika viwango vya ubora vya soka duniani ambavyo hutolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA lakini imeendelea kuburuza mkia kwa nchi za Afrika Mashariki.

Uganda bado wameendelea kuwa vinara kwa nchi za Afrika Mashariki wakishika nafasi ya 13 kwa Afrika na 63 duniani wakifuatiwa na Kenya wanashika nafasi ya 25 Afrika na 98 duniani huku Rwanda wakifuatia katika nafasi ya 27 Afrika na 101 Duniani.

Burundi ndio wanafuatia kwa kuwa nafasi ya 33 Afrika na 112 duniani huku Tanzania wakiburuza mkia kwa kushika nafasi ya 42 kwa Afrika.

Kwa upande wa Afrika Ivory Coast wameendelea kukaa kileleni kwa nchi za Afrika wakikwea mpaka nafasi ya nafasi ya 19, wakifuatiwa na Algeria ambao wameporomoka kwa nafasi mbili mpaka ya 28, Ghana ni wa tatu katika nafasi ya 33.

Kwa upande wa orodha hizo duniani, Ubelgiji bado wameendelea kukaa kileleni mwa msimamo wakifuatiwa na Argentina waliokwea kwa nafasi moja huku Hispania nao wakikwea katika nafasi ya tatu kuwaondoa Ujerumani ambao wameporomoka mpaka nafasi ya nne na Chile wamebaki nafasi yao ya tano waliyokuwepo mwezi uliopita.

Mwandishi Mkongwe Wa Michezo Afariki Dunia
FIFA Yaendelea Kutikiswa Na Jeshi La Polisi Uswiz