Serikali ya Tanzania imesema kuwa inajiondoa katika mpango wa Umoja wa Mataifa wa kuwasaidia wakimbizi kuanza maisha mapya katika mataifa yanayowahifadhi.
Tanzania ambayo imekuwa ni eneo salama kwa wakimbizi wengi na kwasasa inahifadhi zaidi ya wakimbizi 250,000 kutoka Burundi ambao wametoroka mgogoro uliopo nchini humo.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa taifa lake linajiondoa kutokana na tatizo la usalama pamoja na kifedha
Mwaka uliopita Tanzania ilisimamisha kwa muda usajili wa wakimbizi wapya na kuwataka wakimbizi wa Burundi kurudi nyumbani, hatua ambayo ilishtumiwa na makundi ya kupigania haki za kibinaadamu.
Hata hivyo, UNHCR imesema kuwa huo ni mzigo mkubwa kwa Tanzania lakini kwa bahati mbaya, nchii hiyo haipati fedha za kutosha kuwahudumia wakimbizi na wengine wanaotafuta hifadhi.