Marais wa soka wa FIFA na CAF wamesema kuwa wamefuralhishwa na kulikubali soka la Tanzania.
Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Soka Duniani ‘FIFA’, Gianni Infantino akizungumza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa wakati wa uzinduzi wa mashindano mapya ya Ligi ya Soka Afrika ‘AFL’, Dar es salaam alisema soka limekuwa ikiunganisha watu pamoja na hilo limedhihirika nchini Tanzania.
Alisema mashindano ya AFL ni michuano mipya, ambayo italeta msisimko zaidi katika soka la Afrika.
Naye Rais wa Shirikisho la Soka Afrika ‘CAF’, Patrice Motsepe alisema kuwa amefurahi kuona ufunguzi unafanyika Tanzania na mashabiki wameonesha kuwa wanaupenda mpira kwa jinsi walivyojitokeza kwa wingi uwanjani.
Alisema kuwa amelikubali soka la Tanzania na ndio maana uzinduzi huo wameamua kuufanyia katika ardhi la Tarzania.
“Karibu sana leo ni siku maalumu kwenye historia ya mpira wa miguu Tanzania, leo tunaenda kuonesha watu wa Tanzania na Afrika na dunia nzima mpira mzuri wa Tanzania.
“Kumbuka miaka michache kutoka sasa tutaenda kuzindua michuano mikubwa barani Afrika nchini Tanzania, tunaenda kushuhudia timu mbili kubwa na bora barani Afrika acha nianze kwa kuwatakia kila la kheri Simba,” alisema Motsepe.
“Lakini pia nawatakia kila la kheri timu bora na nzuri kutoka nchini Misri Al Ahly karibuni na sasa kwa namna ya kipekee natoa shukrani kwa kaka yangu Rais wa Zanzibar tafadhari karibu, lakini pia namshukuru Waziri wa michezo Damas Ndumbaro na kwa kipekee ni mshukuru Rais Wallace Karia.
“Kabla ya kumkaribisha kaka yangu acha nianze na kaka zangu Mohamed Dewji na mkuu wa msafara wa Al Ahly sasa naenda kumalizia kuna mambo mawili, moja Tanzania inaenda kuandika historia ya kuandaa mashindano ya Afcon mwaka 2027.
“Sasa ngoja nimkaribishe kaka yangu aliyefanya kazi nyingi bila kuchoka na moja ya watu wenye mchango Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani FIFA, Gianni Infantino.
“Simba nguvu moja karibu Tanzania, This is Simba, “alianza kusema Rais Gianni Infantino na kupokelewa kwa nguvu na mashabiki waliojaa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Katika hotuba yake fupi alisema soka limekuwa likiunganisha watu pamoja na hilo limedhihirika jana nchini Tarnzania wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo ya AFL, michuano mipya, ambayo italeta msisimko zaidi katika soka la Afrika.