Tanzania imepata neema kubwa ya soko la saruji kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na zile za Jumuiya ya Maendeleo kusini mwa Afrika (SADC) baada ya nchi hizo kuiomba Tanzania izalishe saruji kwa wingi ili zije kununua.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Innocent Bashungwa kwenye ziara ya kukagua hali ya uzalishaji viwanda vya saruji na kuangalia changamoto zinazo wakabili.

Aidha Waziri Bashugwa ametembelea kiwanda cha kuzalisha saruji cha Camel, kilicho Mbagala jijini Dar es Salaam, ambapo amesema Tanzania ina viwanda 13 vya saruji ambavyo vina uwezo wa kuzalisha tani millioni 10.6 kwa mwaka na mahitaji ya ndani yanafikia tani milioni sita hivyo kuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi.

“Kwenye uzalishaji wa viwanda tuko vizuri sana na tunazidi kufanikiwa na ndiyo sababu wenzetu wameona nchini kwetu kuna fursa ya kununua saruji kwasababu kwa sasa tunaziada ya kuuza nje. Tunamshukuru Rais John Magufuli kwa maono yake makubwa kwenye sekta hii” Amesema Bashugwa.

Aidha Waziri Bashugwa amemuagiza Katibu Mkuu wa wizara hiyo Profesa Riziki Shemdoe kukaa na wenye viwanda ili kuangalia wanavoweza kuwekeza mikoa mingine na kama kutakuwa na chanagamoto wazitatue.

Banki tatu zaunganza kukuza wigo wa mikopo
Magufuli: Jengeni viwanda