Argentina wameng’angania nafasi yao ya juu katika viwango vipya vya FIFA vya dunia – mbele ya mabingwa wa dunia wa sasa nchi ya Ujerumani.

Argentina ambao walifika fainali ya Copa America mwezi Julai kabla ya kupoteza kwa penalti dhidi ya Chile ambayo imekamata nafasi ya tisa baada ya kidondoka nafasi moja.

Katika viwango vipya vilivyotolewa na  FIFA hii leo: nafasi ya kwanza ni Argentina,Germany imeshika nafasi ya pili baada ya kupanda nafasi moja,nafasi ya 3 ni  Belgium ambayo imedondoka nafasi moja, huku Portugal ikikamata nafasi ya 4 baada ya kupanda kwa nafasi mbili,nafasi ya 5 ni Colombia iliyodondoka nafasi 1, Spain imekamata nafasi ya 6 baada ya kupanda kwa nafasi 5 katika viwangio hivi vipya, Brazil imedondoka nafasi mbili na sasa ni ya 7,Wales ni ya 8 ambayo imepanda kwa nafasi 1 ,Chile imedondoka nafasi 1 na sasa ni ya 9, England imesalia katika nafasi yake ya 10.

Kwa upande wa Tanzania inayoongozwa na mzawa Charles Boniface Mkwasa, imepanda kwa nafasi nne na sasa iko katika nafasi ya 136 katika viwango hivyo vipya vilivyotolewa hii leo na Shilikisho la soka Duniani FIFA.

Kwa upande wa Afrika mashariki Uganda inaongoza katika ukanda huu ikiwa katika nafasi 75 kidunia,na imedondoka kwa nafasi 4,ikifuatiwa na Rwanda nafasi ya 93 kidunia ikiwa imedondoka pia kwa nafasi 15.

Ya Tatu Afrika Mashariki ni Burundi baada ya kupanda kwa nafasi 21 na ni ya 113 kwa duniani.Kenya ya nne kwa A.mashariki ikiwa iko nafasi ya 131 wa dunia,na Tanzania ni ya tano na ya mwisho Kwa upande wa Afrika Mashariki ikiwa nafasi ya 136 kidunia ikipanda kwa nafasi nne katika viwango vipya vilivyotolewa hii leo na Shilikisho la soka Duniani FIFA .

Malawi (The Flames) ambayo itacheza mchezo wa kuwania kufuzu fainali za kombe la dunia za mwaka 2018 dhidi ya timu ya taifa ya Tanzania ni ya 101 kwa dunia ikiwa imedondoka nafasi 5, Na Nigeria imepanda nafasi mmoja na sasa ni ya 52 kwa dunia.Timu ya soka ya Nigeria inayoongozwa na kocha Sunday Oliseh, ilicheza mchezo wa kwanza wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017,dhidi ya Timu ya Taifa ya Tanzania  Septemba 05,na timu hizo kwenda sare ya bila kufungana.

Lowassa Atangaza Neema Ya Siku 100 Za Serikali Yake
Malinzi Afunga Kozi Ya Waamuzi Wa FIFA