Tanzania imeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa kamati ya hati za utambulisho ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN Credentials Committee), New York Marekani kwa mwaka 2020/2021.

Hii ni mara ya kwanza katika Historia ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kushika nafasi ya kuongoza kamati hiyo nyeti ya Umoja wa Mataifa, ambapo uteuzi wake ulipendekezwa na Ofisi ya Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa na kuidhinishwa kwa kauli moja na wajumbe wote tisa wa kamati hiyo.

Akizungumza mara baada ya uteuzi huo Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Prof. Kenedy Gaston amesema kuwa uteuzi huo ni muhimu sana na ni ishara ya namna Tanzania inavyokubalika katika uso wa Jumuiya ya Kimataifa.

Balozi Prof. Kenedy Gaston ameongeza kuwa kwa mara ya kwanza tangu uteuzi huo, Tanzania imeongoza kikao chake cha kwanza cha kamati hiyo Kikao kilichofanyika New York, Marekani.

Wajumbe hao ni Marekani,China,Urusi,Cameroon,Uruguay Iceland Papua Guinea, Trinidad, Tobagona na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wabunge 19 viti maalum CHADEMA waapishwa
Tanzania yaithibitishia Jumuiya ya kimataifa kuendelea kulinda amani