Katibu Mtendaji wa Jumuiya ya SADC, Dkt. Stergomena Lawrence ameipongeza Tanzania kuwa nchi pekee ambayo imeongoza kwa kukidhi vigezo vya ukuaji wa uchumi, kwa kufikia asilimia 7, ikiwa ni tofauti na nchi nyingine.

Kauli hiyo ametoa wakati wa mkutano wa kwanza wa SADC uliofanyika jijini Dar es salaam, ambapo viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo wakiwemo viongozi wastaafu na Mawaziri waliohudhuria.

”Uhimilivu wa uchumi ni nyenzo muhimu katika maendeleo, nchi wanachama zimekizi vigezo vya SADC kiuchumi, takwimu zimeonyesha Tanzania inafanya vizuri, na kwa vigezo pekee vilivyoifanya kuwa nchi pekee ambayo imefikia ukuaji wa asilimia 7,”amesema Dkt. Lawrence

Aidha, Dkt. Stergomena Lawrence amesema kuwa katika kufikia uchumi wa Viwanda nchi wanachama hawana budi kukuza uzalishaji wa umeme, kwa kuwa ni kitu muhimu kwenye ujenzi wa viwanda. pia ameishukuru wiki ya Viwanda, ambapo kuna tume ambazo zimeonekana kupitia Mradi wa Umeme wa Nyerere.

Mkutano huo unafanyika kwa siku 2 kuanzia leo Agosti 17 pamoja na Agosti 18.

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake SADC asisitiza ajira kwa vijana
Mgodi wa dhahabu wa GGM kuwanufaisha wananchi