Shirikisho la soka duniani (FIFA) limetoa orodha mpya ya viwango vya ubora wa mchezo huo kwa nchi wanachama.

Katika orodha hiyo Tanzania imeshuka kwa nafasi nne kutoka nafasi ya 135 mwezi Aprili mpaka nafasi ya 139 kwa mwezi Mei ambao umeisha juzi Jumatano.

Kwa Afrika Mashariki, Uganda bado inashika nafasi ya kwanza, duniani ipo nafasi ya 71 ikifuatiwa na Kenya (74) , Rwanda (128), Tanzania (139) na Burundi (148).

Nafasi ya kwanza duniani bado inaendelea kushikiliwa na Brazil ikifuatiwa na Argentina, Ujerumani, Chile, Colombia, Ufaransa, Ubelgiji, Ureno, Uswizi, Hispania na Poland.

Kwa Afrika Misri bado ipo kileleni, lakini kwa upande wa viwango vya dunia ipo nafasi ya 20 ikifuatiwa na Senegal (27), Cameroon (32), Nigeria (38), Congo DR (39) na Ivory Coast (47).

Nchi za Somalia na Tonga zimeshika mkia kwa kukamata nafasi ya 206.

?Live: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Juni 2, 2017
Video: JPM apiga tena, Majaliwa apoza sakata la mchanga wa madini