Tanzania imetajwa kuwa kivutio kizuri cha safari za watalii barani Afrika kulingana na utafiti uliofanywa na mtandao wa SafaricBookings.com ambao ndio ni mtandao mkubwa wa ukuzaji wa safari za Afrika.
Mtandao huo ulifanya tathmini ya zaidi ya wataalam 2500 wale walioshiriki katika safari hizo kabla ya kutangaza kuwa Tanzania ndio eneo bora la safari mwaka 2017 hivyo mtandao huo ulibaini kuwa Tanzania ilipata umaarufu huo kutkana na kuwa na wingi wa wanyama waliopo katika mbuga zake.
Aidha, hivi karibuni baadhi ya watu maarufu duniani wamekuwa wakimiminika kuingia Tanzania kwaajili ya kutembelea maeneo mbalimbali ya kitalii, baadhi ya watu hao ni mwanamuziki maarufu wa Marekani, Usher Raymond, aliyekuwa mchezaji wa Manchester United na Real Madrid, David Bekham, mchezaji wa Liverpool, Mamadou Sakho, mchezaji wa Everton Morgan Schneiderlin na nyota wa filamu kutoka Marekani Will Smith na Harrison Ford.
-
Video: Serikali kula sahani moja na waliokula fedha za ushirika
-
Prof. Maghembe aapa kula sahani moja na majangili
Hata hivyo, mtandao huo pia uliitaja nchi ya Zambia kuwa ni taifa lenye kivutio kizuri cha misitu huku wataalam wote wakikubaliana kwamba mazingira ya misitu nchini humo ni mazuri zaidi.