Tanzania imekuwa mshindi wa tatu na kupata Tuzo za Taasisi zinazosimamia Biashara Duniani, 2020 (WTPO Awards 2020) katika kipengele cha matumizi bora ya ushirikiano katika huduma ya kliniki ya Biashara inayosimamiwa na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade).

Tuzo hiyo imetangazwa Oktoba 14, 2020 jijini Geneva nchini Switzerland ambapo Tanzania imewakilishwa  na Balozi Maimuna Kibenga Tarishi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika ofisi za Umoja wa Mataifa- Geneva.  

Tuzo hizo zinazosimamiwa na kutolewa na Kituo cha Biashara cha Kimataifa Duniani (ITC) ili kutambua michango ya Taasisi zinazosimamia sekta ya biashara duniani (TPO) katika kusaidia Wafanyabiashara wadogo na kati (SMEs) kuimarisha uzalishaji bora wa bidhaa zao, kuwajengea uwezo wa kufanya biashara na kuweza kuuza bidhaa wanazozalisha nje ya nchi. 

Tuzo hizo hutolewa kila baada ya miaka miwili ambapo Tanzania kwa mara ya kwanza kupitia Taasisi ya TanTrade imekuwa mshindi wa Tatu akitanguliwa na Sweden na Viet Nam 

Katika kipengele cha matumizi bora ya ushirikiano nchi nyingine zilizoshiirki katika kundi hilo ni Colombia, Misri, Uholanzi, na Zimbabwe ambazo ziliingia kwenye kwenye mchujo wa mwisho. 

RC Dar awataka wananchi kufuatilia taarifa zinazotolewa na TMA
Producer S2Kizzy avamiwa na kupigwa

Comments

comments