Timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 Ngorongoro Heroes imetwaa taji la CECAFA baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kenya.

Ushindi huo unaipa rasmi Tanzania ubingwa wa CECAFA  ambao mashindano yake yalikuwa yanafanyika nchini Uganda.

Bao hilo pekee limepatikana mnamo dakika ya 46 ya kipindi cha kwanza kwa Otieno Onyango kujifunga.
Tanzania ilifanikiwa kuingia hatua ya fainali kwa kuifunga sudan kwenye mchezo wa awali ambapo katika robo fainali pia Tanzania iliwaondosha Uganda ambao ndio walikua wenyeji wa michuano hiyo.
Baada ya ushindi huo, Ngorongoro wanatarajia kurejea nchini kuanzia kesho.
Video: Tanzania yatwaa ubingwa CECAFA, Kelvin John aweka rekodi mbili kwa mpigo
Video: Hii ndiyo njia ya kuuza madini ya TIN nje ya nchi