Umoja wa Afrika (AU) umezitaka nchi wanachama wa umoja huo kutilia mkazo azimio la kuondoa na kutokomeza silaha haramu ili kuondokana na migogoro inayolifanya Bara la Afrika kushindwa kusonga mbele kiuchumi.

Akifungua Mkutano wa 14 wa dharura wa Umoja wa Afrika uliofanyika kwa njia ya mtandao (Virtual Conference), Mwenyekiti wa Umoja huo ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amesema ni vigumu Bara la Afrika kupiga hatua za kimaendeleo kiuchumi endapo suala la usalama halitapewa kipaumbele na kuruhusu migogoro kuendelea.

Rais, Ramaphosa ameongeza kuwa wakati umefika kwa nchi za afrika hususani zilizopo katika migogoro na vita kuhakikisha kuwa zinatatua vyanzo vya machafuko hayo na kuboresha hali ya kiuchumi kwa wananchi, utawala wa sheria, na kuzingatia misingi ya haki na utawala bora.

Akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli katika mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi amesema mkutano huo ulikuwa unajadili mpango na mkakati wa miaka 10 iliyopita wa kuondoa na kutokomeza silaha haramu na kujenga amani katika bara la Afrika.

“Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeunga mkono azimio la nchi za AU kuongeza miaka mingine 10 ya kutokomeza silaha haramu na kusisitiza tena ushiriki wake kikamilifu katika kuhakikisha kuwa Afrika inatatua migogoro yake yote yenyewe bila kuingiliwa na nchi za nje, lakini pia kuzitaka nchi za Afrika kuzuia mitafaruku na migogoro yote ambayo kwa miaka mingi imeigharimu sana bara la Afrika,” amesema Prof. Kabudi.

Prof. Kabudi ameongeza kuwa, toka hatua ya kuondoa na kutokomeza silaha haramu ilipoanza mwaka 2017 hadi 2019, silaha zaidi ya 1,233 zimerejeshwa na Serikali itaendelea na jitihada ya kuhakikisha kuwa inazitambua sila

Pamoja na mambo mengine, Umoja wa Afrika umekubaliana kuongeza muda wa kuondoa na kutokomeza silaha haramu na kujenga amani katika bara la Afrika kwa kipindi cha miaka 10 ijayo kuanzia mwaka 2021 hadi 2030.

Tanzania, Namibia zakubaliana kuimarisha sekta za Uvuvi na Mifugo
Mino Raiola achafua hali ya hewa Old Trafford