Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo Novemba 27, 2021 amepokea Rais wa Serikali ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni ambapo wamekutana na kufanya mazungumzo na kuja baadhi ya makubaliano katika Maendeleo ya nchi zote mbili.
Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Mkoani Dar es Salaam, Rais Samia Amesema kuwa katika mazungumzo Yao wamekubaliana kuendelea kukuza na kuimarisha uhusiano ambapo wamewaagiza mawaziri wa nchi zote mbili kukutana mara kwa mara na kutatua changamoto zinazojitokeza.
Aidha ushirikiani wa kibiashara baina ya nchi umeongezeka kutoa Bilioni 200 mwaka 2014 na kufikia Bilioni 607 kwa mwaka 2020, huku wakikubaliana kwa pamoja kuondoa vikwazo vya biashara visivyokuwa na Kodi.
Kwa pamoja wamewaagiza mawaziri wa biashara kukutana ndani ya miezi miwili na kujadili jinsi ya kuondoa vikwazo hivyo.
Sambamba na hayo yote Rais Samia amemuomba Rais Museveni vifaa vyote vya ujenzi wa Bomba la mafuta kupitia bandari ya Dar es Salaam ambapo itakuwa ni fursa yakuendelea kukuza mapato kupitia bandari.