Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Handeni Tanga na waziri wa Viwanda wa Biashara, Abdallah Kigoda amefariki leo majira ya saa kumi jioni, katika hospitali ya Appolo, India alipokuwa akitibiwa.

Taarifa rasmi kuhusu kifo chake zimetolewa leo jioni na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Taarifa zaidi juu ya msiba huu, ikiwa ni pamoja na taratibu za kuusafirisha mwili wa Marehemu na mipango yote ya mazishi zitaendelea kutolewa na serikali pamoja na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya Marehemu kadri zitakavyoendelea kupatikana,” ilieleza taarifa hiyo ya Ofisi ya Bunge.

Mh. Kigoda amekuwa waziri wa pili kufariki katika kipindi hiki cha uchaguzi ikiwa ni siku chache baada ya Taifa kumpoteza aliyekuwa waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Bi. Celina Kombani.

Dar24 inatoa pole kwa familia ya Marehemu, jamaa na marafiki. Mungu awape faraja na nguvu katika kipindi hiki kigumu. Apumzike kwa Amani.

 

Picha: Lowassa Azidi Kutikisa, Mwanza Yazizima Kumlaki… Aahidi Meli Mpya
Balaa Laendelea Kuikumba Man City