Askari wanane wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wamefariki katika ajali mbili tofauti zilizotokea jana jijini Dar es Salaam na Mkoani Kigoma.

Taarifa zilizotolewa jana na jeshi hilo, zimeeleza kuwa askari wawili, Luteni Kanali Kilikisa Ndongoro na Kapteni Gaudencia Khamis walipotea katika Bahari ya Hindi baada ya ndege waliyokuwa wanaitumia kwa mafunzo maalum kuanguka.

Msemaji wa JWTZ, Kanali Ngeleba Lubinga alieleza kuwa askari hao waliruka kutoka kwenye ndege waliyokuwa wakifanyia mafunzo maalum kwa lengo la kujiokoa baada ya ndege hiyo kupata hitilafu katika injini.

Kanali Lubinga alieleza kuwa askari hao walifanikiwa kuruka kwa kutumia parachute lakini kwa bahati mbaya waliangukia bahari ya Hindi na kupotea majira ya saa tatu asubuhi, katika eneo la Kisiwa cha Mbudya.

Aidha, wanajeshi sita wa Kambi ya Bulombola, Kigoma wameripotiwa kufariki baada ya basi walikokuwa wakisafiria kupata ajali majira ya saa 10 jioni katika eneo la mlima Pasua, lililopo kati ya wilayani Uvinza na Kigoma Mjini.

Mashabiki England Washangaa Sturridge Kuachwa
Jaji Lubuva Achoshwa Na Chadema, Awataka Wazibe Madirisha…