Mwanamuziki nguli wa muziki wa Dansi, Ramadhani Masanja maarufu kama Banza Stone amefariki dunia leo mchana (Julai 17) katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam alipokuwa akipata matibabu.

Taarifa za kifo chake zilithibishwa na kaka yake, Jabir Masanja alieleza kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na fangasi kichwani kwake na kwamba dawa kali alizokuwa akitumia zilimsababisha kukosa hamu ya kula.

Naye mnenguaji wa bendi ya Twanga Pepeta aliyewahi kufanya kazi pia na Banza Stone alieleza kuwa alipomtembelea marehemu katika siku za mwisho za uhai wake, aligundua kuwa mbali na kuzorota kwa afya yake alikuwa ameanza kupoteza pia ufahamu. Mama mzazi wa marehemu aliwahi kueleza hivi karibuni kuwa mwanae alikuwa anagoma kula chakula mara kadhaa kutokana na kukosa hamu ya chakula.

Enzi za uhai wake, marehemu Banza Stone alitamba kwa mitindo mbalimbali ya rap zake hasa alipokuwa na bendi ya ToT, wimbo wa ‘Mtaji wa Masikini’ ni moja kati ya nyimbo zake kubwa alizowahi kufanya.

Dar 24 inaungana na ndungu, jamaa na marafiki katika kipindi hiki kigumu. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amina.

Ne-Yo Amtafuta Diamond Afrika Kusini, Wapanga Collabo
Inspector Haroun Ajibu Tuhuma Za Kumdhurumu Luten Karama Na Kumbania