Jaji mstaafu, Robert Kisanga amefariki dunia Katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI).
Taarifa hiyo imethibitishwa na Rais wa Chama cha Majaji Wastaafu, Thomas Mihayo.
Kisanga aliwahi kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufaa, pia amewahi kuwa mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora kabla ya kustaafu mwaka 2008.
Anakumbukwa kwa hukumu ya Nyamuma. Kesi ya haki za binadamu ilifanywa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora wakati yeye akiwa Mwenyekiti wa Tume huyo.
Aliyekuwa Rais wa wakati huo, Benjamin Mkapa aliipinga hukumu hiyo na Serikali haikutekeleza maagizo yoyote juu ya waathirika wa Nyamuma waliochomewa nyumba, uchomaji ulioongozwa na Marehemu Mabiti aliyekuwa DC wa kipindi hicho.