Jaji mkuu mstaafu wa Tanziana Augustino Ramadhani afariki dunia leo, Aprili 28 Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kweye ukurasa wa Twitter wa Mahakama Kuu, Jaji Ramadhani amefariki saa mbili asubuhi katika hospitali ya Agha Khan baada yakuugua kwa muda mrefu.

Ikumbukwe Jaji Ramadhani aliwahi kuwa Brigedia Jenerali kabla ya kuitwa katika sekta ya Sheria na kutumikia Mahakama.

Lakini pia ndiye alikuwa Mtanzania wa kwanza kushikilia kiti cha Urais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu tangu kuanzishwa kwa Mahakama hiyo.

Kim Jong-un azungumza kwa mara ya kwanza tangu azushiwe kufa
GGML yatoa Sh bilioni 1.6 kuunga mkono mapambano dhidi ya Corona