Aliyekuwa mbunge wa viti maalum kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Leticia Nyerere amefariki dunia majira ya saa mbili jana usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Taarifa za uhakika zinaeleza kuwa Leticia Nyerere alifariki katika hospitali ya Doctors Community iliyoko Lah Ham, MaryLand Marekani alipokuwa akipatiwa matibabu.

Julai 27 mwaka jana, Marehemu alitangaza kuihama Chadema na kuhamia CCM.

Dar24.com inaungana na watanzania wote kutoa pole kwa familia yaMwalimu  Nyerere pamoja na watanzania kwa ujumla kutokana na msiba huu. Apumzike kwa amani. Amina!

Mchumiatumbo Kuzichapa Na Benk Mwakalebela
Maalim Seif apigilia Msumari Rasmi Zanzibar, Apinga Kauli za CCM