Mchungaji wa Kanisa la Mlima wa Moto, Mama Gertrude Rwakatare amefariki dunia leo, Aprili 20, 2020 majira ya Alfajiri.

Mtoto wake, Muta Rwakatare amethibitisha taarifa hizo alipozungumza kupitia kipindi cha Super Breakfast cha East Africa Radio.  

Kwa mujibu wa mwanaye, mama Rwakatare alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya moyo, hivyo kwa taarifa za awali inaweza kuwa chanzo cha kifo chake.

“Ni bahati mbaya imetokea asubuhi ya leo saa 11 kasoro, alikuwa na matatizo ya moyo, jana tulimkimbiza Hospitali lakini bahati mbaya imetokea, tupo katika hatua ya kuangalia namna gani tutafanya ili tuweze kumpumzisha mama yetu,” Muta ameiambia East Africa Radio.

Askofu huyo alikuwa mbunge wa kuteuliwa, amefariki akiwa na miaka 70 .

 Enzi za uhai wake aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum (CCM) kuanzia mwaka 2008 hadi 2015, na baadaye mwaka 2017 Lwakatare aliteuliwa kwa mara ya pili kuwa mbunge wa viti maalum kujaza nafasi ya mama Sofia Simba aliyevuliwa uanachama wa CCM.

Pia Marehemu Mama Rwakatare ndiye muanzilishi wa shule za st. Mary’s International schools.

Pierre Liquid aambukizwa Corona bar
Wagonjwa 23 wa corona waongezeka Zanzibar, vifo viwili