Mgombea ubunge wa jimbo la Lushoto, Tanga kwa tiketi ya Chadema, Mohamed Moti, amefariki baada ya kupata ajali ya gari.

Katibu wa Chadema wilaya ya Lushoto, Abdalah Dhahabu amethibitisha kifo cha mgombea huyo na kueleza kuwa ajali hiyo ilitokea jana jioni wakati mgombea huyo alipokuwa akitoka katika kampeni zilizofanyika katika eneo la Mlola.

Akieleza sababu ya kutokea kwa ajali hiyo, alisema wakati wakiwa njiani kuelekea nyumbani kwa marehemu baada ya kumaliza kampeni, gari hilo liliacha njia.

Katibu huyo wa Chadema alieleza kuwa dereva wa gari hilo lilipata ajali alikimbizwa hospitali na anaendelea vizuri.

 

Magufuli Kuwaneemesha Wafanyakazi
Wafikishwa Mahakama Ya Kisutu Kwa Makosa Ya Mtandao