Rapa Michael Dennis Mhina, maarufu kama Joni Woka, alipata umaarufu zaidi kwa kurap kama mlevi, amefariki leo alfajiri katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu.

Msanii huyo aliyekuwa akiunda kundi la ‘Watukutu’ akiwa na Ras Lion, alipata ajali ya kulipukiwa na mtungi wa gesi juzi na kukimbizwa katika hospitali hiyo.

Mtu wa karibu wa rapa huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa ajali hiyo ilitokea wakati John Walker alipokuwa akijaribu kurekebisha gari lao akiwa na wenzake katika moja ya garage eneo la Sinza jijini Dar es Salaam.

“katika kuhangaikia upande wa AC mtungi wa gas ukalipuka,moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani. Madaktari wanahofia imefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo,” alielezea.

Kwa yeyote aliyeguswa na angependa kutoa rambi rambi anaweza kuwasiliana na kaka yake kwa namba +255767007005.

Dar24 inatoa pole kwa ndugu, jamaa pamoja na wadau wa muziki nchini.

Apumzike kwa Amani. Amina!

Msanii wa Afrika ashinda Tuzo ya Grammy kwa mara ya tatu
Takukuru kutumbuliwa tena, Waziri asema anaweza kuwafuta wote