Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Maunda Zorro amefariki dunia kwa ajali ya gari
Maunda aliyewahi kutikisa kwenye bongofleva kupitia nyimbo zake kadhaa ikiwemo ‘Nataka niwe wako’ na Mapenzi ni ya wawili’ amekumbwa na umauti usiku Aprili 13.
Kwa mujibu wa Banana Zorro ambaye ni kaka wa marehemu, mdogo wake alifariki kufuatia ajali ya gari iliyotokea saa chache baada ya kuachana naye.
Banana ameeleza kuwa aliachana na Maunda saa 12 jioni baada ya kujumuika kwenye msiba wa rafiki yao wa muda mrefu.
Taarifa za awali zinaeleza kuwa gari alilokuwa akiendesha Maunda liligongana na lori la mchanga na kusababisha umauti wake.
Saa nne usiku baada ya kuachana naye alipata taarifa za ajali na kifo cha mwanamuziki huyo kutoka kwenye familia ya mwanamuziki Zahir Ally Zorro.
Endelea kufuatilia Dar24 Media Kwa Taarifa Zaidi