Kiungo wa klabu ya Simba, Mohammed Ibrahim amepata pigo baada ya kumpoteza mtoto wake wa kiume aliyefariki dunia usiku wa kuamkia jana katika hospitali ya mwananyamala iliyopo jijini Dar es salaam.

Klabu ya Simba pamoja na mashabiki wa klabu hiyo wameungana na Watanzania wengine kumpa pole kiungo wao kwa pigo kubwa alilopata kumpoteza mtoto wake wa kiume ambaye alilazwa katika hospitali hiyo ambapo jitihada za madaktari kuokoa maisha ya mtoto huyo mdogo kugongwa mwamba.

Afisa habari klabu ya Simba, Haji Manara ametumia ukurasa wake wa instagram kutoa rasmi taarifa hiyo na kumpa pole kiungo huyo wa Simba.

 Serikali yaitaka Halmashauri ya Kongwa kutenga fedha za Umeme
Dr.Shika: Simfahamu Babu Seya

”Klabu ya Simba inatoa pole kwa kiungo wetu ‘Mohammed Ibrahim’ kwa kufiwa na mwanae mpendwa, tumeumia sote kwa msiba huu wa mtoto wetu mdogo kabisa. Klabu ya Simba inatoa pole kwa msiba huu mzito kwako na kwa famila nzima. Inna lillah wainna ilaihi Raajiun” alisema taarifa ya Simba .

Mungu aipumzishe roho ya malaika huyo kwa amani.

 

 

Nkurunzinza kuiongoza Burundi hadi 2034?
CCM yafuta mchakato kura za maoni Singida Kaskazini