Muigizaji maarufu wa Kenya, Benson Wanjau maarufu kama Mzee Ojwang amefariki Jumapili jioni katika hosptali ya ‘Kenyatta National Hospital’ alipokuwa akitibiwa.

Muigizaji huyo wa vipindi vya ucheshi alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa Pneumonia. Aliopotea katika vipindi vya runinga kwa muda mrefu na kujikita katika matibabu ya afya yake.

Enzi za uhai wake, Mzee Ojwang alitamba kwa ucheshi wake kupitia vipindi vingi vya runinga vikiwemo Vitimbi, Vituko, Vioja Mahakamani na Kinyonga.

Tunawapa pole ndugu jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu. Mungu ailaze roho ya Mzee Ojwang mahala pema peponi.

Mila Kunis Aithibitisha Ndoa Na Ashton Kutcher Na Kumiliki Bunduki
Matokeo Rasmi: CCM Yampa Magufuli Ridhaa kwa kishindo