Aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Jonathan Shana amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Taarifa iliyotolewa na hospitali ya taifa ya Muhimbili mapema leo imeeleza kuwa Kamanda Shana amefariki katika hospitali hiyo alipokuwa akipatiwa matibabu kwa takriban wiki tatu sasa.

Shana alifahamika zaidi katika kujihusisha na shughuli za Vyama akiwa na sare za kipolisi. Aidha, aliwahi kufananisha Chama Tawala, Serikali na Dola kwa Kanuni za Kihesabu.

Kamanda Shana aliwahi kuwa RCO Mikoa Mbalimbali Nchini ikiwemo Simiyu, RPC-Mikoa ya Pwani, Mwanza na Arusha

ACP Jonathan Shana amefariki akiwa Afisa Mnadhimu Namba Moja katika Chuo cha Polisi (CCP) Moshi.

Mfumo wa 'BONASI' wabadilishwa Young Africans
Picha: Aubameyang amaliza ukimya kwa vitendo

Comments

comments