Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi, Dkt. Augustine Mahiga amefariki dunia leo, Mei Mosi, 2020 akiwa jijini Dodoma.
Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeeleza kuwa Balozi Mahiga aliugua ghafla akiwa nyumbani kwake na alifikishwa hospitalini akiwa tayari ameshafariki.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ametuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; Wabunge na Wafanyakazi wa Wizara ya Sheria na Katiba.
“Pamoja na umri wake mkubwa na uzoefu wa kushika madaraka katika nyadhifa, Marehemu Balozi Mahiga alikuwa mnyenyekevu na mtiifu kwa kila jukumu nililomtuma,” amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amesema kuwa anaungana nao katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.
Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani. Amina!
Undani wa kisa cha mwanamke aliyewapikia mawe watoto wake na muujiza uliotokea