Hatimaye Shirikisso la Soka Tanzania ‘TFF’ limeweka wazi tarehe maalum za michezo ya minne ya Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Tanzana Bara ‘ASFC’ msimu huu 2022/23.

TFF imetangaza tarehe maalum za michezo hiyo, baada ya kupangwa kwa Droo ya Robo Fainali mwishoni mwa juma lililopita kwa kushirikiana na Wadhamini wakuu Kampuni ya Azam Media.

Taarifa iliyothibitisha tarehe za michezo hiyo imetolewa katika vyanzo vya habari vya Shirikisho hilo, leo Jumatatu (Machi 20).

Mabingwa watetezi wa ‘ASFC’ Young Africans watacheza dhidi ya Geita Gold jijini Dar es salaam April 08, ikiwa ni siku chache baada ya kurejea nchini ikitokea DR Congo, itakapokwenda kucheza mchezo wa mwisho wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya TP Mazembe.

Simba SC ambayo imepangwa kukutana na Ihefu FC itacheza mchezo wake wa Robo Fainali jijini Dar es salaam April 07, baada ya kurejea nchini ikitokea Morocco itakapocheza mchezo wake wa mwisho wa Kundi C, Ligi ya Mabingwa Barani Afrika dhidi ya Raja Casablanca.

Azam FC itacheza dhidi ya Mtibwa Sugar April 03 katika Uwanja wa Azam Complex Chamazi, jijini Dar es salaam, huku mchezo kati ya Singida Big Stars dhidi Mbeya City ukipangwa kupigwa April 02 mjini Singida kwenye Uwanja wa Liti.

Msaada wa maafa: Rais Chakwera aishukuru Tanzania
Rais Samia azindua Programu Kilimo mashamba makubwa