Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Nchini – TARI, imekabidhi msaada ya pembejeo za Kilimo kwa waathirika wa maafa ya maporomoko ya mawe na tope kutoka mlima Hanang’.

Msaada huo uliokabidhiwa hii leo Desemba 13, 2023 ni Mbegu za Maharage kilo 400, Alizeti kilo 100 pamoja na mbegu za Ngano kilo 300 zitakazowasaidia Wakulima ambao mashamba yao yameathiriwa na maafa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mbegu hizo, Mkurugenzi wa Utafiti na Ubunifu – TARI, Dkt. Furaha Mrosso pia ametoa salamu za pole kwa Serikali na waathirika wote, huku akisema wameamua kuleta mbegu Daraja la msingi zenye ubora, ili walime na kujipatia chakula kwa wingi.

“Tumetoa mbegu hizi ili kuleta nafuu kwa wakulima waliopata madhara ya maafa kutokana na uharibifu wa mazao uliosababishwa na maafa, tutaendelea kufanya hivi kadri inavyowezekana,” alieleza Dkt. Mrosso.

Naye Mkurugenzi Msaidizi Huduma za Ugani kutoka Wizara ya Kilimo, Dkt.Upendo Mndeme akimwakilisha Katibu Mkuu wa Wizara hiyo amesema kwa kuzingatia madhara ya maafa hayo ikiwemo uharibifu wa mashamba wamechangia mbegu hizo zitakazozalisha haraka.

Akitoa neno la shukran mara baada ya kupokea msaada huo, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Dkt. Jim Yonazi amewapongeza TARI kwa kuwashika mkono Wakulima wa Hanang waliofikwa na maafa hayo na kueleza msaada huo utawafikia wote na kutumika kama ilivyokusudiwa.

Habari kuu kwenye Magazeti ya leo Desemba 14, 2023
Maxi: Young Africans inakwenda Robo Fainali