Mdau wa Soka la Bongo Abbas Tarimba amesema anapata ushawishi mkubwa kutoka kwa wadau wenzake ili agombee Urais wa TFF.

Tarimba ambaye ni mbunge wa Jimbo la Kinondoni kupitia tiketi ya CCM, amesema ushawishi huo amekua akiupata kwa njia ya simu.

Amesema pamoja na ushawishi mkubwa unaomuelemea kwa sasa, bado hajafanya maamuzi kama ataingia kwenye uchaguzi wa TFF ama la.

Amesema anatambua wazi ana haki ya kuwani nafasi ya uongozi ndani ya TFF, kwa kuwa katiba ya Shirikisho hilo inamtaka mwenye sifa kuu ya uraia wa Tanzania.

“Nimekuwa nikipokea simu kutoka kwa watu mbalimbali kunitaka kugombea Urais wa TFF, lakini binafsi bado sijafanya maamuzi, mimi ni Mtanzania na nina haki ya kufanya hivyo acha niangalie nikiona inawezekana nitajua cha kufanya,” Abbas Tarimba.

Uchaguzi mkuu wa TFF umepangwa kufanyika jijini Tanga mwezi Agosti mwaka huu, huku kamayi ya uchaguzi ikitoa wito kwa wadau wa soka kujitokeza kwa wingi ili kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Shirikisho hilo.

Wamangituka alikana jina lake
Karia achukuliwa fomu TFF