Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania – TASAC, limefanikiwa kuongeza idadi ya kadhia zilizohudumiwa kutoka kadhia 6,000 mwaka 2019/2020 hadi kufikia kadhia 10,000 mwaka 2022, kuunda nyenzo za udhibiti wa usafiri majini pamoja uundaji wa Kanuni na Miongozo, ili kuwezesha utekelezaji wa sheria katika kudhibiti usafiri majini.
Hayo yamebainishwa jijini Dar es Salaam na Kaimu Kaimu Mkurugenzi wa TASAC, Nelson Mlali katika semina ya Wahariri wa vyombo vya Habari iliyoratibiwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina na taja miongoni mwa fursa hizo kuwa ni pamoja na usajili wa meli kwa masharti rafiki, uanzishwaji wa maeneo ya ukarabati na ujenzi wa meli katika Ukanda wa Pwani.
Amesema, “kuongezeka kwa idadi ya leseni za vyombo vidogo ambapo hadi sasa vimefikia 6,366 huku kazi ya kuongezeka kwa idadi ya vyeti kwa mabaharia waliokidhi masharti ambao wamefikia 17, 689 ambao wanafanyakazi nchini na wengine Serikali imewapelaka nje ya nchi kwa ajili ya kusomea kazi ya ukaguzi wa meli za kimataifa.”
Aidha, Mlali amesema wamefanikiwa kuongeza idadi ya watoa huduma wanaodhibitiwa na TASAC, kwa maana ya idadi ya leseni na vyeti vya usajili vilivyotolewa,pamoja na kuongezeka kwa idadi ya vyeti kwa mabaharia waliokidhi masharti na kuimarisha udhibiti wa huduma za bandari baada ya urasimishaji wa maeneo 20 ya kibandari katika mwambao wa bahari na maziwa.
“Utekelezaji wa Mikataba ya Kimataifa kuhusu, Usafirishaji Majini inayoratibiwa na Shirika la Bahari Duniani (International Maritime Organization – IMO), Kufanya ukaguzi wa meli zilizosajiliwa nchini na meli za nje zinazoingia katika bandari za Tanzania Bara, Kudhibiti vivuko (Ferries),” amesema Mlali.
Kwa mujibu wa Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura ya 415, majukumu makuu ya TASAC yapo kwenye vifungu Na. 7, 11 na 12 ikiwamo kufanya kazi za Uwakala wa Forodha (Clearing & Forwarding Function) kwa bidhaa chache zenye maslahi mapana kwa Taifa na ilianzishwa chini ya Kifungu cha 4 cha Sheria ya Uwakala wa Meli Tanzania, Sura ya 415 na kuanza rasmi kutekeleza majukumu yake Februari 23, 2018 kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 53 lilitolewa Februari 16, 2018.