Mpango wa kunusuru Kaya masikini (TASAF) wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala umetoa jumla ya shilingi milioni 292 kwa ajili ya kusaidia kaya masikini 6115 za wilaya hiyo.
Fedha hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Saalam na Mratibu wa TASAF wa Halmashauri hiyo, Mwaluma Msofe ambaye amesema kuwa fedha hizo zitagawanywa kwenye mitaa 74 ya Halmashauli hiyo ndio walengwa wa mpango huo.
Msofe ameongeza kuwa mchakato wa kuwapata wananchi wenye maisha magumu unafanywa na wananchi wenyewe katika mtaa husika ambapo baada ya kuwatambua  wanathibitishwa mbele ya mkutano wa mtaa.
“Fedha tunazowapatia wananchi hawa zimeanza kuonyesha mafanikio kwa kuwa zimesaidia kaya hizo kuanzisha miradi midogo midogo inayowawezesha kuendeleza maisha yao pia fedha hizo zimesaidia watoto kupata mahitaji muhimu ya shule hivyo kupelekea mahudhurio kuongezeka”, alisema Msofe
Mratibu huyo amefafanua kuwa kuna aina mbili za ruzuku ambazo ni ruzuku ya msingi ambayo kaya masikini hupewa kwa mtu yeyote anayetambuliwa na mpango huo wakati ruzuku ya masharti hutegemea na aina ya familia.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kimanga- Darajani, Chacha Mwenge amesema kuwa anaendelea na kazi ya kusimamia na kuchambua majina ya wahusika kwa kuwa kuna baadhi ya wananchi waliingizwa katika mpango huo bila kuwa na sifa kutokana na wananchi hao kutoa taarifa za uongo                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                                             “Tumegundua kuwa kuna baadhi ya kaya ambazo  zimeingia kwenye mpango huu kimakosa kwahiyo tunaendelea kuzitoa, hadi sasa jumla ya kaya 28 za mtaa wetu tumeshaziondoa kwa sababu ya kukosa sifa”, alisema Mwenge.

Naibu Waziri Wa Ujenzi Mhandisi Ngonyani Akanusha Tuhuma Za Kumchafua Raisi Magufuli
Waziri Wa Ujenzi Profesa Mbarawa Azindua Train Stesheni Mpaka Pugu