Chama cha Mchezo wa Karate Tanzania (TASHOKA) kinaendelea kutekeleza kwa vitendo matukio katika kalenda yake ya Mwaka 2022 iliyoitoa hivi karibuni.
Kwa mujibu wa Kalenda hiyo Kuanzia February 12 mpaka April 16 mwaka huu kunafanyika Semina elekezi kwa wakufunzi wote wa vilabu vya TASHOKA pia kunafanyika kozi ya uamuzi wa Karate Grade D, C na B.
Katibu mkuu wa Chama cha Mchezo wa Karate Tanzania Sensei Jerome Mhagama, amesema sehemu zitakazohusika na semina na kozi hizo ni Dar es Salaam, Singida na Iringa.
“Kalenda hiyo ni rasmi ya Tanzania Shotokan-Ryu Karate-DO Association (TASHOKA) itakayo tumika kwa kipindi chote cha Mwaka-2022.”
“Kwa kuzingatia kuwa Kalenda nyingi za Mashirikisho ya Kimataifa bado hazijawa tayari mpaka hivi sasa na kwa kawaida Kalenda nyingi za Mashirikisho hayo zinatoka mwezi Machi-2022, hivyo basi yapo matukio mengi ya Kimataifa ambayo hayapo katika Kalenda kwa sasa.”
“Kwa msingi huo kama Taifa tunaweza kupata mualiko wa tukio lolote la Kimataifa ambalo halipo katika Kalenda kwa sasa na kupelekea mabadiliko ya Kalenda yetu kwa wakati wowote kuanzia mwezi Machi, na hii itakuwa kwa yale matukio yenye tija kwa Taifa tu.” amesema Sensei Jerome Mhagama