Tasnia ya Habari nchini, inatarajiwa kuendeshwa kitaaluma kitu ambacho kitafanya watu kuiheshimu na kuacha tabia ya kujitolea Habari au kuongea chochote bila kufuata misingi na taratibu husika kwani wanaotakiwa kufanya hivyo ni Vyombo vya Habari ambavyo vinatambulika kisheria.

Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Eng. Kundo Mathew wakati akiongea na Dar24 hivi karibuni na kusema wanaotakiwa kutoa habari ni vyombo vile ambavyo vitambulika kwa mujibu wa sheria za Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Eng. Kundo Mathew.

“Sasa hao tunaposema wanaenda kuendesha kitaaluma, ina maana watazingatia weledi na maarifa ya uandishi wa Habari kusudi taarifa inapotoka kwenda kwa mlaji au mwananchi basi iwe inakidhi vigezo, ubora na viwango vinavyotakiwa,” amesema Kundo.

Aidha, ameongeza kuwa mabadiliko hayo ya sheria ya Habari yanalenga kunyanyua sekta hiyo kiuchumi kwani vyombo vingi vya Habari vimekuwa vikijiendesha bila faida licha ya kuwa maandalizi ya utafutaji wa kazi za kuiarifu jamii yana gharama.

West Ham United wanaisubiri Arsenal
Mbadala wa Bares kutangazwa Tanzania Prisons