Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limetoa wito kwa wajasiriamali kuchangamkia fursa iliyotolewa na Serikali kwa kuanzisha viwanda ili kuongeza kasi ya ukuaji wa uchumi nchini.

Akizungumza katika hafla ya utoaji leseni na vyeti kwa wajisiriamali katika Ofisi za Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania Mhandisi Johanes Maganga amesema, TBS imetoa vyeti na leseni 303, ambapo leseni na vyeti 163 sawa na asilimia 54% vimetolewa kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, na vyeti na leseni 139 sawa na asilimia 48% vimetolewa kwa wajasiriamali wengine.

Amesema Vyeti na leseni hivyo vinahusisha bidhaa mbalimbali kama vile chakula, vipodozi, viati, vifaa vya ujenzi, vifaa vya umeme, vifaa vya makenika, magodolo, vibebeo, pamoja na vifungashio.

Aidha Shirika limeendelea kutenga bajeti ya kuwasaidia wajasiriamali wadogo kuanzisha viwanda na kupata leseni ya kutumia alama  ya ubora katika bidhaa zao bure. Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Shirika limetenga jumla ya shilingi 256,000,000 kwa ajili ya kuwahudumia wajasiriamali wadogo”. Amesema

Nae Kaimu Mkurugenzi wa Udhibiti Ubora TBS, Baraka Mbajije amesema vyeti na leseni vilivyotolewa na Shirika hilo vitaongeza imani kwa watanzania kuwa bidhaa zao ni salama na zinakidhi matakwa ya viwango.

Amesema Vyeti na leseni vilivyotolewa vitasaidia bidhaa kukubarika sokoni kwasababu zitakuwa tayari zinaaminika ubora na usalama wake.

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania Mhandisi Johanes Maganga akikabidhi vyeti na leseni kwa wazalishaji wa bidhaa nchini katika hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania Mhandisi Johanes Maganga akizungumza katika hafla ya utoaji leseni na vyeti vya ubora kwa wazalishaji wa bidhaa kwenye hafla iliyofanyika kwenye Ofisi za Makao makuu ya TBS Jijini Dar es Salaam.

DC akanusha kuibwa viungo vya marehemu
Ibrahim Ame: Fiston Mayele ni NOMA