Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), Hamza Johari, amefafanua sababu iliyopelekea, kuzizuia Ndege za Kenya kutua nchini mara baada ya nchi hiyo kuzuia ndege za Tanzania kutua kwao.

Akizungumza na East Afrika Radio katika kipindi cha Super Breakfast amesema kuwa nchi ya Kenya ilikuwa imeomba ruhusa ya Ndege zake kutua nchini kuanzia leo, lakini wao walishangazwa kuona Kenya yenyewe imezuia ndege za Tanzania

“Tumefikia uamuzi huo kwa sababu katika sheria na taratibu zinazosimamia uendeshaji wa usafiri wa anga kati ya nchi na nchi ni kwamba, Mataifa yanatakiwa yawe sawa kwa sawa, Kenya walikuwa wameomba kuja Tanzania kuanzia leo kutua katika viwanja vya Dar es Salaam, Zanzibar na Kilimanjaro na sisi hatukuwa na tatizo tukawapa ruhusa, lakini baadaye tukasikia wao wanatuzuia sisi tusiende kule” amesema Johari.

“Mwaka 2015 walizuia gari za watalii zisiingie Kenya, kwahiyo tukafanya hivyo na baada ya siku mbili wao wakaondoa kikwazo walichotuwekea, tumetendewa kitu ambacho si sahihi na sisi inabidi tufanye hivi badala ya kukaa kimya na kuwaacha wao waendelee kufanya wanachotaka”amesema Johari

Kwa mujibu wa kipindi cha kipindi cha Super Breakfast Waziri wa Uchukuzi wa Kenya, James Macharia amsema “Hakuna ndege ya Tanzania ambayo imezuiliwa kuingia Kenya, sisi tulisema hizo nchi tulizoziweka kwenye hiyo orodha watu wao wakifika hapa hawatakaa karantini, lakini kama nchi haipo kwenye hiyo orodha watawekwa Karantini, sisi taarifa ya kuzuiwa kuingia Tanzania tumeipata lakini tutazungumza na wenzetu na tutasikilizana”

Fainali ASFC: Matola, Hitimana watambiana
Ndege za Kenya zapigwa ''stop'' Tanzania