Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), inatarajia kufanya majaribio ya kwanza ya mfumo wa rada ya kuongozea ndege nchini unaojengwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).
 
Hayo yamesemwa na Msimamizi wa Ujenzi wa jengo hilo, Steven Mwakisasa alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mara baada kutembelea jengo hilo jijini Dar es salaam, ambapo amesema kuwa ujenzi wa jengo hilo umekamilika na ufungaji wa vifaa unaendelea hivyo ifikapo Desemba 21 wataweza kufanya majaribio.
 
“Kama mnavyoona wanahabari kila kitu kimeshafanyika tunachomalizia ni mitambo midogo midogo inayotarajia kukamilika ifikapo wiki ijayo na tufanye majaribio ili kuona ni wapi pa kurekebisha au tuongeze kitu gani?,” amesema Mwakisasa.
 
Kwa upande wake, mwongoza Ndege Mkuu wa TCAA, Justine Ncheye amesema kuwa mara baada ya kukamilika na kuanza kufanya kazi, mfumo huo utaimarisha zaidi ulinzi wa anga la Tanzania.
 
Aidha, amesema kuwa kwa kiasi kikubwa rada hiyo pamoja na zile zitakazojengwa Mwanza, Songwe na Kilimanjaro zitasimamiwa na TCAA ikiwamo kuziongoza ili kuhakikisha ulinzi unaimarishwa zaidi.
 
  • Serikali yatoa milioni 500 ujenzi wa hospitali Wanging’ombe
 
  • Benki ya TPB yaandaa mkutano wa mabenki ya Akiba Afrika Mashariki
 
  • Majaliwa afungua kiwanja kipya cha Baseball jijini Dar
 
Hata hivyo, Jiwe la msingi la ujenzi wa mfumo huo wa rada liliwekwa Aprili 2, 2018 na Rais John Magufuli na utagharimu Sh. 67 bilioni zikijumuisha mfumo wa rada uliojengwa katika viwanja vya ndege vya Mwanza, Kilimanjaro na Songwe

Video: Membe atua usiku kikachero, Lowasa afunguka hatima yake Chadema
JPM ampa shavu Msekwa na wastaafu wengine watano