Eva Godwin – Dodoma.
Tume ya Maendeleo ya Ushirika nchini – TCDC, imelenga kuimarisha Maendeleo ya Ushirika huku ikijipanga katika mwaka 2023/2024 kutekeleza maeneo saba ya Kimkakati yatakayolenga kufikia kipaumbele hicho cha kuwekeza mifumo ya kisasa ya kidijitali.
Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma, Mrajisi wa Vyama vya Ushirika na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege amesema uendelezaji huo unalenga kuongeza ufanisi wa kiutendaji katika Vyama vya Ushirika na Mamlaka za Usimamizi.
“Na pia eneo jingine ni kuharakisha mchakato wa uanzishwaji wa Benki ya Taifa ya Ushirika ili kuviwezesha Vyama vya Ushirika kupata Mikopo yenye Riba nafuu,Kuhamasisha mfumo wa Ushirika kujiendesha kibiashara wenye kuaminika na shindani ukijikita kwenye mkkuongeza thamani ya uzalishaji katika Vyamawa,” amesema Ndiege.
Aidha, amesema wataboresha Sera, Sheria na usimamizi wa Ushirika ili kuchochea ukuaji na maendeleo ya Ushirika imara nchini na kuendelea kuhamasisha Ushirika kwenye sekta mbalimbali na makundi maalum, ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wananufaika na mfumo wa Ushirika.