Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew ameitaka Mamlaka ya Mawasiliano nchini – TCRA, kufanyia kazi malalamiko ya wananchi kuhusu utapeli unaoendelea kujitokeza kwa watumiaji wa simu za mkononi.

Kundo ameyabainisha hayo Bungeni jijini Dodoma wakati akijibu swali la nyongeza la mbunge wa viti maalumu Zuena Baushir aliyetaka kujua ukomo wa tatizo hilo linaloendelea kuwakabili wananchi.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Kundo Mathew.

Mapema mwaka huu (2023), TCRA ilizima laini za simu ambazo hazijahakikiwa kama sehemu ya jitihada za Serikali kudhibiti utapeli kupitia simu za mikononi.

Huu hapa wasifu wa Kocha Youssouph Dabo
ASFC-Simba SC yaitangazia vita Azam FC