Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetengeneza kanuni ndogo zitakazoratibu  utoaji wa huduma ya vifurushi zinazotolewa na kampuni mbalimbali za simu nchini ikiwa ni njia ya kukabiliana na malamiko juu ya huduma hizo.

Akizungumza leo Machi 2, 2021 Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,  James Kilaba amesema utekelezaji wa kanuni hizo utaanza Aprili 2, 2021.

Aidha Kuandaliwa kwa kanuni hizo kumekuja kufuatia maoni  3278 yaliyotolewa na wananchi kuhusu vifurushi hivyo.

Amesema kuwa Miongoni mwa yaliyoelekezwa kwenye kanuni hizo ni huduma zote za vifurushi lazima zipate vibali vya TCRA huku mamlaka hiyo pia ikitoa mwongozo wa bei zilizowekwa na mamlaka hiyo.

Nyingine ni  vifurushi vyote havitaondolewa au kurekebishwa ndani ya miezi mitatu baada ya kuidhinishwa.

Pia, mtoa huduma atatakiwa kutoa taarifa kila wakati matumizi ya kifurushi yatakapifikia asilimia 75 kabla ya kuisha na kitakapomalizika kabisa kwa asilimia 100.

Wanafunzi waliotekwa waachiwa huru
Azam FC yatua kibabe Kagera