Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Valeria Msoka amesema kuwa katika hali ya kusikitisha na kustaajabisha, baadhi ya vyombo vya habari vilisambaza picha za ajali iliyotokea mkoani Morogoro.

Amesema kuwa vyombo vya habari hivyo hususani ‘Online TV’ zaidi ya 15 zilichapisha na kutumia picha mbalimbali za miili ya watu waliofariki katika ajali kinyume na kanuni, miiko na maadili ya uandishi

Baadhi ya Viongozi wa vyombo vya habari walikiri makosa hayo na kuomba radhi mbele ye Kamati ya Maadili ya TCRA walipoitwa kuhojiwa.

Viongozi wa Lemutuz Online TV na Global TV, vituo vilivyochapisha picha hizo, walifika mbele ya Kamati Agosti 28 kwa kushindwa kujirekebisha ndani ya muda wa Kanuni

Le Mutuz ilieleza kuwa kosa hilo lilisababishwa na uzembe wa Msimamizi wao wa maudhui ambaye hakutumia busara na weledi katika uchapishaji wa video ile.

Aidha, Global TV ilisema kuwa ilichukua tahadhari kubwa ya kuziziba picha kwa kuweka kivuli lakini kulitokea tatizo la kiufundi na picha hizo zikaonekana.

Hata hivyo, baada ya utetezi wa viongozi hao wa Kamati ya maudhui ilivipa onyo kali chaneli hizo na kuziamuru kuomba radhi kupitia chaneli hizo kwa siku 7 mfululizo kuanzia Septemba 07.

Mrithi wa Tundu Lissu ala kiapo Bungeni, Janga la vipodozi bandia
LIVE: Rais Magufuli katika mkutano na wadau wa sekta ya ujenzi Tanzania