Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),  imewataka watoa huduma ya habari mtandaoni kuhakikisha wanaandika habari kwa usahihi na bila kuegemea upande wowote hususani katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Tanzania mwaka 2020.

Kisaka ameyasema hayo leo Septemba 15,2020 wakati akitoa mada kuhusu Kanuni za Utangazaji wakati wa uchaguzi za mwaka 2015 kwenye Mkutano wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Watoa Huduma ya Habari Mitandaoni ‘Online Content Service Providers’ uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu  Julius Nyerere (JNICC),  jijini Dar es salaam.

 “Muwe makini mnapoandika habari, usiegemee upande mmoja, unaporipoti hakikisha hujaongeza mtazamo wako,usiongeze ongeze maneno yako, hakikisha unawapa nafasi sawa wagombea wote wa vyama vya siasa”,amesema Mhandisi Kisaka.

“Usitoe nafasi kwa mgombea anayetumia lugha kali na chafu inayoweza kuhatarisha amani ya nchi, kamwe chombo chako cha habari kisitumike kuhamasisha au kuonesha kitu cha hovyo, ukiona kitu cha hovyo unaweza kukatisha matangazo”,amesisitiza Kisaka.

Akifungua mkutano huo, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dkt. Wilson Charles Mahera amewashukuru watoa huduma ya habari mitandaoni kwa ushirikiano wao na kuwataka kuvipa nafasi sawa vyama vyote vya siasa na kuepuka kuandika habari zenye kuhamasisha vurugu na kusababisha uvunjivu wa amani. 

Aidha, Dkt. Mahera amesema mkutano huo umefantika kwa lengo la kuwajengea uelewa watoa huduma ya habari mtandaoni kuhusu mkachato wa uchaguzi ili waweze kuelimisha jamii kuhusu taratibu mbalimbali za uchaguzi pamoja na kuhamasisha wananchi kujitokeza kwenda kupiga kura Oktoba 28,2020.

Tanzania yaongoza ukuaji uchumi kipindi cha Covid-19
Guardiola awaburuza England, awapiga bao Ole, Mourinho

Comments

comments