Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amewataka Watanzania kuwapuuza matapeli wanaotumia mitandao ya Internet na Simu za mikononi, kwa kuwaomba wawatumie fedha kupitia mitandao hiyo.
Ameyasema hayo Jijini Mwanza kwenye mkutano wa siku moja wa wadau wa mawasiliano ambapo amesema kuwa wananchi wanapokuwa wanakutana na hali hiyo wanatakiwa kuripoti kwenye mtandao husika wa simu kisha TCRA.
Amesema kuwa kwasasa kuna wimbi kubwa la matapeli ambalo limekuwa likiwarubuni wananchi kutuma kiasi cha fedha kupitia mitandao ya simu za mikononi.
“Njia moja ya kuweza kuwakwepa matapeli hawa ni kutoa taarifa kwa wamiliki wa mitandao ya simu wanayotumia, baadaye kutoa taarifa kwetu, sisi kama TCRA hatukai kimya, tunashughulika na changamoto hizi,”amesema Kilaba
Hata hivyo, katika hatua nyingine, Kilaba amewakumbusha watoa huduma kuhakikisha kwamba wanapata leseni itakayowawezesha kuendelea kutoa huduma kwenye vyombo vya utangazaji ikiwemo udukuzi na utumiaji wa taarifa kupitia mitandaoni.
-
Kigwangalla ashangazwa na watanzania wanaosubiri kuajiliwa, ‘Maisha hayakusubiri’
-
Mbowe aweka hadharani kinachomsumbua
-
Mbuga tatu za wanyama Tanzania zatajwa kuwa bora zaidi Afrika 2018