Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kituo cha televisheni, Wasafi TV, kwa muda wa miezi sita kuanzia Januari 6, 2021, hadi Juni 2021 kwa makosa ya kukiuka taratibu za utangazaji.

TCRA imesema kituo hicho kimekiuka kanuni za utangazaji kwa kurusha maudhui yaliyomuonesha mwanamuziki Gigy Money akionesha utupu wake akiwa jukwaani.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu Mkurugenzi wa Sheria wa TCRA, Kaimu Mkurugenzi wa Sheria wa TCRA, Johanes Kalungula , amesema kuwa mamalaka iliwataka kituo cha wasafi kufika na kutoa maelezo kwanini wasichukuliwe hatua za kisheria kwa kukiuka sheria na taratibu za utangazaji.

”TCRA imeamua kuanzia muda huu wa agizo hili mpaka mwisho wa siku ya leo wasafi Tv watakiwa kuomba radhi kwa watanzania kwa kukiuka kanuni za utangazaji kupitia kipindi cha Tumewasha Live Concert” amesema Kalungula. 

”TCRA imesitisha utoa wa huduma za utangazaji za wasafi tv kwa muda wa miezi 6 kuanzia January 6, 2021 mpaka Juni 6 2021, iwapo Wasafi TV itashindwa, kukataa au kukaidi uamuzi huu hatua zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi ya Wasafi TV” amesema Kalungula. 

Maamuzi hayo yanakuja kufuatia maudhui ya picha jongefu yaliyomuonesha msanii wa Bongo Fleva, Gift Stanford, maarufu kama Gigy Money akicheza utupu kinyume na kanuni za maadili katika tamasha la Tumewasha Live Concert lililorushwa Januari Mosi 2021 kuanzia saa mbili hadi saa tano usiku.

Hakuna kuingia wala kutoka Kigali
Gutteres alaani shambulio la Niger