Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa itawachukulia hatua za kisheria wamiliki wa vyombo vya habari mtandaoni yaani Blogs, tovuti, TV za mtandaoni ambao wanaendelea kukiuka sheria ya usajili wa vyombo hivyo na kuendelea kuweka habari.

Hayo yamesemwa leo Septemba 11, 2018 na Mhandisi wa TCRA, Francis Mihayo wakati wa semina ya wadau mbalimbali iliyoandaliwa na TCRA.

”Wapo ambao bado wanaendelea kuweka habari, video na vitu vingine ilihali hawajasajiliwa lakini niwaambie kuwa kufanya hivyo ni kinyume na sheria, hivyo wakati ukifika tutawakamata kwa sasa tunawaangalia tu maana tunawaona wote na kile wanachokifanya” amesema Mihayo

Ikumbukwe kuwa, mnamo Aprili , 2018 TCRA ilitoa muda wa wiki mbili kwa wamiliki wa vyombo vya habari mtandaoni kujisali ili kuweza kupata kibali cha kuendesha vyombo hivyo, wapo waliotii amri hiyo kama Dar24 Media na vyombo vingine, lakini pia wapo waliokiuka agizo hilo na kuendelea kurusha maudhui yao bila usajili kinyume na sheria.

 

Mwanamitindo alivunjia heshima vazi la utawa, adai ni sanaa
Chadema waiombea njaa CUF, "Kikitetereka sisi tutaimarika zaidi"