Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), na wadau mbalimbali wa habari imewaasa wamiliki na watumiaji wa mitandao ya kijamii kuwa makini na namna ya upashaji wa habari za mitandaoni.

Kupitia agizo hilo, TCRA pamoja na wadau wa habari wamekubalina kuandaa sheria na taratibu zitakazo ongoza namna bora ya utumiaji wa mitandao ya jamii kwa lengo la kuhabarisha.

Hivyo kwa taratibu hizo itakuwa rahisi kwa TCRA, kupambana na changamoto za upashaji habari kwa njia ya mitandao ya kijamii.

Mwenyekiti wa kamati ya Maudhui TCRA, Valerie Msako ametaja baadhi ya chanagamoto katika mitandao ya kijamiii zikiwemo ongezeko la waandishi wa sio na taaluma na kuanzishwa kwa runinga za mtandaoni (onlineTVs).

Ambapo Kupitia runninga na kuwepo waandishi wasio na weledi kumepelekea uvunjifu mkubwa wa maadili ya habari, kwani kumekuwa na usambazaji wa habari nyingi zinazopotosha umma.

‘Teknolojia ya habari imetoa fursa ya kila mtu kuwa chanzo cha habari. Kuwa chanzo cha habari inatakiwa ifanywe kwa tahadhari. Maadili ya uandishi hayaruhusu kusambaza habari zinazokuwa na maudhui yasiyofaa’, Amesema Valerie

Aidha moja ya wadau wa habari na Mkurugenzi wa Jamii Forums, Maxence Melo ameitaka TCRA kuandaa utaratibu maalumu wa kudhibiti wavunjifu wa maadili ya habari kama ilivyokuwa kampeni ya Futa Delete kibisa.

Pia ameomba TCRA kushirikiana na watumiaji wa mitandao ya kijamii ili kuisaidia kukabiliana na matatizo yanayotokea mtandaoni.

 

Jorge Celico abebeshwa zigo la kufuzu kombe la dunia
Chadema yaomba msaada Ujerumani, EU matibabu ya Lissu