Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA imewataka wateja visimbuzi vya DSTV, ZUKU na AZAM kutuma taarifa zao zinazoonesha na kuthibitisha kuwa wamekuwa wakilipia chaneli za ndani jambo ambalo ni kinyume na sheria.

TCRA imewataka wateja wa ving’amuzi hivyo kutoa taarifa juu ya majina yao kamili yaliyosajiliwa katika king’amuzi, aina ya king’amuzi anachotumia, namba ya kadi ya king’amuzi chake, eneo alipo, kiasi cha pesa ambacho amekuwa akilipia kutazama chaneli hizo na idadi ya miezi aliyolipia.

Taarifa hiyo ni maalumu kwa mtazamaji aliyekuwa anatozwa kutazama chaneli za televisheni ya TBC 1, ITV, STAR TV, CHANNEL TEN, EAST AFRIKA TV, na CLOUDS TV.

TCRA imewataka wahanga hao kutoa taarifa hizo ofisini kwao kupitia barua pepe au barua ya kawaida kwenye anuani yao ya dg@tcra.go.tz au kupitia kwa Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Mawasiliano kwa sanduku la Posta 474.

Mnamo Agosti 7, 2018 Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania iliziamuru Kampuni za DSTV, AZAM TV na ZUKU kuondoa cheneli za kutazamwa bila kulipia baada ya kukiuka sheria na masharti ya leseni zao kwa kuwatoza watazamaji ada za viwango mbalimbali kutazama chaneli hizo ambazo kisheria zinapaswa kutazwa bure.

 

Abdoul 'Razza' Camara aombwa kustaafu soka
Upinzani Rwanda washinda uchaguzi kwa mara ya kwanza