leo Agosti 28, 2020 Mamlaka ya mawasiliano Tanzania TCRA imeipa adhabu kampuni ya Raha Limited inayojihusisha na usambazaji wa mtandao chini  kulipa billion 11.8   kwa kosa la kukiuka sheria za mawasiliano.

TCRA imesema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikitumia masafa ya 1452-1482 MHZ  bila ya kuwa na kibali kuanzia machi 24 mwaka huu .

Pia TCRA  imeipa kampuni ya Raha Limited adhabu ya kulipa milioni 40  kwa kushindwa kusambaza huduma za mtandao , kushindwa kutoa ripoti ya fedha ,mpango kazi  wa mwaka kwenye rasilimali watu pamoja kushindwa kuomba upya kibali kwa muda muafaka .

“Ngoja niweke sawa jambo hili, kutumia masafa ni jambo nyeti sana kiusalama ndiyo maana hakuna mtu anaruhusiwa kutumia bila kibali cha mamalaka ,kwahiyo kampuni hii imekiuka sheria za mawasiliano,” Amesema Mkurugenzi mkuu TCRA James Kilaba .

siku za hivi karibuni Raha Limited imejitangaza zaidi kama Raha Liquid Telecom.

Kilaba amesema kuwa Raha inatakiwa kulipa adhabu hiyo ndani ya siku 90 na wakishindwa hatua zaidi zitachukuliwa dhidi yao au kama maamuzi hayakuwa haki  Raha inanafasi ya kukata rufani .

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Agosti 29, 2020
Kigoma kunufaika na mfuko wa maendeleo wa Kuwait