Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeviadhibu vituo vya runinga vya Star TV na Azam TV kwa kutangaza habari bila kufuata misingi ya uandishi wa habari.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Joseph Mapunda amesema kuwa Star TV itatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 7.5 kwa kutangaza habari ambazo hazikuthibitishwa.

Alisema Star TV walirusha habari kutoka katika Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kuwa watu walipigwa katika uchaguzi mdogo wa madiwani, bila kuuliza Jeshi la Polisi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Kadhalika, alisema Azam TV inapaswa kulipa faini ya shilingi milioni 7.5 kwa kutangaza habari za uchochezi kuhusu uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana, bila kuuliza upande wa NEC na Jeshi la Polisi.

Mapunda amesema kuwa faini hizo zinapaswa kulipwa ndani ya kipindi cha siku 30 kuanzia leo.

Picha: Paka wa ajabu azaliwa, ana vichwa viwili na macho matatu
Picha: Zawadi ya Papii Kocha kwa Rais JPM